WELCOME TO ARDHI UNIVERSITY STUDENTS' BLOGSPOT

"OUR PLATFORM"

A WORD........

If you have any question or you have a post and you want us to post it for you please use the contact details below. We guarantee to respond to your query ASAP. However, we discourage abusive language, any thing with inappropriate words will not be attended.

Any comment,opinion or news email: andika2me@gmail.com

BE FREE, BE YOU

Saturday, 4 July 2009

IFM JUU -MISS HIGHER LEARNING

Miss Vodacom Higher Learning 2009/10, Betrice Lukindo (katikati) akiwa katika picha ya pozi na mshindi wa pili, Linda Mzinga (kulia) na kushoto ni Doris Donatus, mshindi wa tatu
------------------------------------------------------------------------------------------------

Chuo cha Usimamizi wa fedha cha IFM cha jijini Dar, kimeibuka kidedea katika Shindano la kumsaka mlimbwende wa Vyuo Vikuu nchini, Miss Higher Learning, baada ya Mwanafunzi wa chuo hicho, Betrice Lukindo, kutwaa taji hilo usiku wa kuamkia leo.Wakati Betrice akibatizwa umalkia wa Vyuo Vikuu nchini, Linda Mzinga kutoka Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama amechukua nafasi ya pili na Doris Donatus kutoka Dar es Salaam Institute of Technology (DIT) akiibuka mshindi wa tatu.Kwa ushindi huo, Magreth amepata tiketi ya moja kwa moja ya kujiunga na Kambi ya Miss Tanzania msimu huu, tayari kwa kuwania taji la Miss Tanzania, 2009/10.Shindano hilo lilifanyika ndani ya viunga vya Karimjee katikati ya jiji la Dar es Salaam, lililosababishwa kwa udhamini mkubwa wa Mtandao wa simu za mkononi wa Vodacom, Global Publishers Ltd, Clouds FM, Ndege Insuarance, kinywaji cha Overmeer na wadhamini wengine kibao.

Juddy.